Kalamu ya Jabir

Kalamu ya Jabir

Katika taaluma ya habari, ujasiri ni mila. Asiye jasiri hana nafasi katika uandishi. Ndivyo tusemavyo. Ujasiri wa Jabir Idrissa ni wa kupigiwa mfano. Kwa zaidi ya muongo mmoja na nusu sasa, Jabir amekuwa akiitumia kalamu yake kusema kauli moja tu, Ndiyo Zanzibar. Haoni haya, haoni tabu wala haogopi kusema hivyo popote pale awapo na katika jukwaa lolote analoitwa.

Ziifuatazo ni baadhi ya makala zake alizoziandikia gazeti la MwanaHalisi la Dar es Salaam, ambalo amekuwa akilifanyia kazi kama mhariri mwandamizi, ambazo zinaakisi kiwango cha juu cha kujitolea kwa mwandishi wa Kizanzibari kwa ajili ya mama yake mpendwa, Zanzibar.

Kampeni ya vurugumechi haina nafasi

KIPINDI cha vurugumechi kimewadia. Zanzibar wakati wa uchaguzi huwa na mambo mengi. Mengi kwelikweli kiasi cha baadhi yake kusababisha kuwachanganya wananchi. Endelea kusoma makala hii

Ya nini ajizi? Mzanzibari sema NDIYO

JUMAMOSI hii – tarehe 31 Julai, siku tatu zijazo – ndiyo siku ya uamuzi kuhusu mustakabali wa Zanzibar na Wazanzibari wenyewe. Hiyo ndiyo siku kwa kila mwananchi kupiga kura ya NDIYO kwenye kisanduku cha kura ya maoni ili kuyapa nguvu maridhiano yaliyoanzishwa na viongozi wetu wakuu katika siasa Zanzibar, Rais Amani Abeid Karume wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Maalim Seif Shariff Hamad wa Chama cha Wananchi (CUF). Hiyo ndiyo siku tunayopaswa kuitumia vizuri nafasi yetu ya haki kwa kusema NDIYO. Endelea kusoma makala hii

Mpinga umoja unaojengwa Z’bar ndiye shetani

MAKADA wa Kisonge wanasema: TANU na ASP ndio walioleta umoja wa kitaifa. Hatudanganyiki; hapana hapana. Endelea kusoma makala hii

Bado nasubiri ‘maridhiano ya kweli’

SHIDA wanazopata wananchi wengi wakati huu awamu ya pili ya uandikishaji wapiga kura Zanzibar ukiendelea, zinaelezea tatizo la msingi liliopo katika uongozi wa nchi. Endelea kusoma makala hii

Migawanyiko CCM inaipeleka Zanzibar kubaya

SAUTI ya Tanzania Zanzibar (STZ), stesheni ya redio inayoendeshwa kwa fedha za wananchi, inamnukuu Waziri Kiongozi, Shamsi Vuai Nahodha akilaumu watu wanaosema kura ya maoni imeshapita. Endelea kusoma makala hii

CCM achieni Zanzibar ijizongoe

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinajenga siasa mbaya. Kwa kinavyoyachukulia baadhi ya mambo muhimu yenye maslahi na taifa, hapana shaka kinaelekea katika kukwamisha maridhiano Zanzibar. Endelea kusoma makala hii

Kura ya maoni inasubiriwa sana Zanzibar

KILA niliyekutana naye na kujadili maendeleo ya kisiasa yanayotokea Zanzibar kipindi hiki, aliniuliza ni nini hasa serikali inachotafuta kutoka “kura ya maoni.” Endelea kusoma makala hii

Zanzibar kupata serikali ya umoja siyo mseto

HARAKATI kwa ajili ya uteuzi wa wajumbe watakaounda timu ya watu sita itakayoratibu utekelezaji wa azimio la Baraza la Wawakilishi, ziko mbioni kukamilishwa. Endelea kusoma makala hii

Karume ampiku Kikwete

RAIS Amani Abeid Karume amepanda chati kisiasa hata kumzidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Endelea kusoma makala hii

Mbinu za Magogoni zinavyojaribiwa majimboni

MALUMBANO kwa wadau wa uchaguzi Zanzibar yamefikia hatua mbaya. Vyama vya upinzani hasa Chama cha Wananchi (CUF) vinaamini watu wapatao 170,000 hawatagusa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) na hivyo hawatapiga kura; matokeo yake itakuwa manufaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kwa Zanzibar, kinatajwa kupoteza kila uchaguzi tangu 1995. Endelea kusoma makala hiiMfumo dume wa uchaguzi unadumaza demokrasia

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Celina Kombani anatamba: “Uchaguzi umefanikiwa kwa asilimia 98.” Endelea kusoma makala hiiNini matarajio ya Jumamosi Pemba?

SIKU 38 baada ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kusitisha uandikishaji kwa ajili ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura (DKWK) la Zanzibar, kazi hiyo inaanza tena Jumamosi 12 Septemba 2009. Endelea kusoma makala hii

Vitambulisho vimeanza kutafuna wakubwa

ZOGO la kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi, sasa siyo tena mgogoro kati ya serikali na Chama cha Wananchi (CUF) pekee. Ni zogo lililotapakaa hadi katika taasisi za serikali. Endelea kusoma makala hii

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s