Hotuba ya Dk Shein Alipozungumza na Waandishi, Wahariri na Wananchi

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein

TAARIFA YA RAIS WA ZANZIBAR NA MWENYEKITI WA BARAZALA MAPINDUZI, MHESHIMIWA DKT. ALI MOHAMED SHEIN, KWA WAANDISHI WA HABARI, WAHARIRI NA WANANCHI KUHUSU HALI YA NCHI, TAREHE 31 MEI, 2012

Ndugu Waandishi wa Habari, Wahariri na Wananchi,

Assalam Aleykum

Namshukuru Mwenyezi Mungu, Mola wa walimwengu wote, kwa kutupa afya njema tukaweza kuzungumzia mambo yenye mustakbal mwema wa hali ya nchi yetu kwa jumla.

Napenda kutanguliza shukurani zangu kwa wananchi wa Zanzibar kwa kuendeleza na kudumisha amani hasa tokea kupatikana kwa maridhiano ya kisiasa baina ya vyama viwili vikuu vya siasa hapa Zanzibar, Chama cha Mapinduzi na Chama cha CUF, yaliyopelekea kuundwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa mnamo Novemba, 2010 kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. Continue reading

Advertisements
Posted in Uncategorized

Wazanzibari wacharuka, wagomea Tume ya Katiba

Jaji Joseph Sinde Warioba, mwenyekiti wa Tume ya Kukusanya Maoni kuhusu Katiba

WANANCHI wa Visiwa vya Zanzibar wamekuja juu na kudai kuwa hawatatoa tena maoni yao mbele ya Tume ya Kukusanya Maoni ya Jaji Joseph Warioba wakipinga kile walichodai kuzuiwa na hatimaye kukamatwa kwa wananchi 12 wa kisiwa cha Pemba, waliotaka kujadili masuala ya Muungano. Continue reading

Posted in Uncategorized

Zanzibar: a sinking tourist paradise

Zanzibar’s Stone Town alley

The tourist island of Zanzibar is celebrating the day of union with mainland Tanzania, while posing a sinking threat, not in the Indian Ocean, but in political turbulence, likely to damage the once famous paradise in East Africa.

Politics is currently dominating every corner of this beautiful tourist island that once earned fame from prominent world personalities including Bill Gates, The Aga Khan, and the famous South African singer, Sipho Mabhuse, who sang in his song, “Oh Zanzibar.”

While tourists are still flocking to Zanzibar’s warm tropical beaches to enjoy the African sun or playing with dolphins and taking the time to go scuba diving, read more…

Posted in Uncategorized

Profesa Sharif: Karume alidhani amesaini Shirikisho la Afrika Mashariki, si Muungano wa nchi mbili

Prof. Abdul Sheriff

WAKATI Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar ukitimiza miaka 48 mwaka huu, kumekuwa na harakati nyingi visiwani Zanzibar za kutaka uhuru mpya wa visiwa hivyo na kuupinga Muungano wazi wazi.

Watu wamekuwa wakijadiliana kupitia kwenye makongamano, mabarazani na hata kwenda mahakamani kutafuta uhalali wa Muungano. Kupitia njia hizo Wazanzibari wametoa sababu mbalimbali za kupinga Muungano. Continue reading

Posted in Uncategorized

Sheikh Karume na kilio cha sasa cha Wazanzibari

Abeid Amani Karume, Rais wa kwanza wa iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

MENGI yameandikwa na mengi yataendelea kuandikwa kumhusu Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa mwanzo na wa pekee wa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambaye Aprili, mwaka 1964 alikubali kuiunganisha nchi yake na ile ya Tanganyika.

Hadi sasa walioandika kumhusu Karume ni waandishi wa habari, wanahistoria na wataalamu wa fani ya sayansi ya siasa. Waandishi wa riwaya hata wa riwaya sahili na wa tamthilia bado hawajajitokeza uwanjani kumuandika Karume. Sitoshangaa pakitokea magwiji watanzu hizi mbili za fasihi watakaoamua kumtoa ukumbini Sheikh Karume kwa kumjadili na kumzungumza ama katika riwaya za kisiasa au katika michezo ya kuigiza. Continue reading

Posted in Uncategorized

Kwa nini Okello alifurushwa Zanzibar?

Field Marshal, John Okello (katikati mbele)

Mwandishi Ahmed Rajab anajaribu kuelezea sababu za kufukuzwa kwa “Field Marshal” John Okello visiwani Zanzibar baada ya mapinduzi ya mwaka 1964. Makala hii ni majibu ya mlolongo wa hoja za mwandishi Joseph Mihangwa juu ya sababu zilizopelekea mwanamapinduzi huyu anayesemekana kuchangia kwa kiasi kikubwa “kufanikiwa” kwa mapinduzi hayo yaliyomuondowa madarakani Sultan Jemshid bin Abdullah. Kufahamu zaidi endelea  kusoma hapa

Posted in Uncategorized

WAZANZIBARI WANA HAKI YA KUJADILI MUUNGANO

Mamia ya Wazanzibari wakiwa katika maandamano ya amani kudai kurejeshwa kwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar

Labda leo makala hii ivunje ukimya juu ya hali ya kisiasa inayoendelea hivi sasa hapa Zanzibar, maana vyombo vya habari vyote vya Tanzania vimefanya kama kwamba hakuna kilichopo, yaani mambo kama kawaida.

Kwa hakika mambo si kama kawaida. Kuna harakati nyingi na ziko wazi kabisa ambazo zinafaa kuandikiwa kwa sababu ni kwa kuandikiwa ndio zitajulikana lakini si kujulikana tu ila hata kufanyiwa uchambuzi. Continue reading

Posted in Uncategorized