Zanzibar Daima

Mohammed Ghassany

Mohammed Ghassany alianza kuonekana katika gazeti la Rai la Tanzania mwaka 2001 na baadaye umaarufu wake ukajengwa katika gazeti la mwanzo huru la Zanzibar, Dira Zanzibar, baina ya mwaka 2003 na 2004. Tangu hapo, makala kadhaa juu ya siasa, uchumi, utamaduni na jamii ya Zanzibar, ambazo zimemfanya aitwe katika  midahalo, makongamano na semina za ndani na nje ya nchi kuwasilisha mtazamo wake kuhusiana na masuala mbalimbali yanoyuhusu Zanzibar.

Anasema katika utangulizi wa weblog yake anayoiita Zanzibar Daima:

“Weblog hii imeanzishwa kwa lengo la kujenga jukwaa la mawasiliano kati ya Zanzibar na ulimwengu kupitia mtazamo wa Kizanzibari. Dhamira ni kuiwasilisha na kuiwakilisha Zanzibar. Imani kuu ni Uzanzibari, ambalo ni jambo la fakhari kwa kila Mzanzibari awe anaishi ndani ya mipaka ya Zanzibar au nje yake.”

Zanzibar Daima ni mkusanyo wa kazi kadhaa za Ghassany, ambamo ameandika kuhusu ushairi, historia, siasa, jamii na uchumi. Muna pia sehemu ya maoni, ambayo mwenyewe anasema ni muhimu sana kwake, ili aweze kujua mawazo ya watembeleaji wake ” hata kama hayaakisi mtazamo wa weblog yenyewe.”

Karibu usome uchambuzi wa kina wa masuala mbalimbali yanayohusu Zanzibar na kisha usisahau kutuma maoni yoyote, ambayo unadhani yanaweza kuisadia Zanzibar.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s